YANGA YAONDOA UKAME

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga SC imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting na kumaliza ukame wa ushindi kwenye ligi.

Katika mchezo huo wa raundi ya 14 bao pekee la Yanga limefunga dakika ya 45 na kiungo aliyesajiliwa kutoka Mbao FC Pius Buswita.

Yanga imepata ushindi wa kwanza mwaka huu baada ya kutoa sare na Mwadui FC katika mchezo wa raundi ya 13 huku mwishoni mwa mwaka 2017 ilipokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Mbao FC ya Mwanza.

Yanga sasa imefikisha alama 25 na kupanda hadi nafasi ya 3 ikizizidi klabu za Singida United yenye alama 23 pamoja na Mtibwa Sugar yenye alama 25 ikitofautiana na Yanga kwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post