WAZIRI WA JPM : ASKOFU KAKOBE ANASUMBULIWA NA UGONJWA WA AKILI

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema kuwa ukimpeleka mahakamani Askofu Zacharia Kakobe atashinda kwasababu watu wanasema inawezekana anasumbuliwa na ugonjwa wa akili.

Kigwangalla ameyasema hayo jana kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter ambapo ameeleza kuwa ugonjwa unaotajwa kuwa huenda unamsumbua Kakobe dalili zake ni kujisifia.

Kigwangalla amefafanua aina ya ugonjwa huo wa akili ambao inawezekana unamsumbua Askofu Kakobe kuwa ni 'Bipolar Disorder: Currently Mania’. Pia amesisitiza kuwa hata ukimpeleka mahakamani anaweza akashinda kwa kigezo hicho.

''Kuhangaika na mtu kama KAKOBE ni kupoteza muda bure. Kuna watu wanasema inawezekana akawa na ugonjwa wa akili ‘Bipolar Disorder: Currently Mania’ ambao katika dalili zake ni ‘delusions of grandeur’ . Akipelekwa mahakamani anaweza kutetewa kwa kigezo hiki na akashinda!'' ameandika Kigwangalla.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.