WASIRA : CHADEMA NDIYO SHETANI WETU


Mwanasiasa mkongwe na aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika katika serikali ya awamu ya nne na mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya CCM, Stephen Wasira amedai hawawezi kufanya siasa bila ya kukitaja chama cha CHADEMA kwa kuwa ndio shetani wao.


Wasira amebainisha hayo leo wakati wa uzinduzi wa kampeni za Ubunge jimbo la Kinondoni zilizofanyika katika viwanja vya Biafra Jijini Dar es Salaam huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba baada ya kusikia kauli ya mgombea Ubunge wa Jimbo hilo katika 'televison' kuwa CCM hawawezi kufanya siasa bila ya kuitaja CHADEMA.

"Nimemshangaa kiukweli mgombea huyo, maana hata Maimamu na Wachungaji huwa hawawezi kumaliza ibada bila ya kumtaja shetani maana shetani ndio mpinzani wao na endapo wasipotaja wana kuwa hawajamaliza ibada yao. Hivyo asishangae sana na sisi tunapokuwa katika siasa kuitaja CHADEMA kwa maana ndio shetani wetu hapa", alisema Stephen Wasira.

Kwa upande mwingine, Wasira amesema tokea mwaka 2015 kumekuwa na siasa za kishetani nchini Tanzania hasa upande wa upinzani ambazo zimetawaliwa na uongo unaofanana na giza kwa kusema uongo katika kampeni zao na kudanganya wananchi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527