WASIOJULIKANA WAPIGA TUKIO KANISANI BILA HOFU YA MUNGU


Watu wasiojulikana wamevunja kufuli na kuingia ndani ya Kanisa la Baraka na Uzima (GRM) lililopo Mtaa wa Kokehogoma Kata ya Turwa wilayani Tarime na kufanikiwa kuiba vitu vya kanisa hilo vyenye thamani ya zaidi ya Sh1.7 milioni.Mchugaji wa kanisa hilo, Ezekiel Ngurumo amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Jumatano Januari 10 ambapo waliibia viti 28, spika, inveta na jenereta vitu vya thamani hiyo.


“Tulishtuka baada kufika alfajiri kanisani kwa ajili ya maombi kama ilivyo desturi yetu ya kila siku na kukuta vitu hiyo vimeibwa,” amesema Mchugaji Ngurumo.

Mchugaji Ngurumo alilaani kitendo hicho na kuwataka wananchi kubadilika na kuwa na hofu ya Mungu kwani vitendo walivyofanya hakijamfurahisha Mungu.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Kokehogoma, Josephat Ndonge amesema alipata taarifa za vitu kuibwa ndani ya kanisa hilo mapema leo Jumatano na kuwataka wananchi kutoa taarifa pale watakaposikia vitu hivyo vikiuzwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/ Rorya, Henry Mwaibambe alikiri kuwepo kwa tukio hilo na kuwataka wananchi kutoa taarifa za wahalifu hao.

Na Dinna Maningo, Mwananchi
Theme images by rion819. Powered by Blogger.