Tuesday, January 30, 2018

WABUNGE WATATU WALA KIAPO BUNGENI DODOMA

  Malunde       Tuesday, January 30, 2018

Wabunge wapya wakila kiapo cha uaminifu bungeni baada ya kuanza kwa kikao cha kwanza cha mkutano wa kumi, mjini Dodoma leo. Kuanzia kushoto ni Dk Damas Ndumbaro wa Jimbo la Songea Mjini, Justin Monko wa jimbo la Singida Kaskazini na Dk Stephen Kisurwa wa Jimbo la Longido. Picha na Edwin Mjwahuzi 
Mkutano wa 10 wa Bunge umeanza leo Januari 30 mwaka 2018 mjini Dodoma kwa wabunge wapya watatu wa CCM kula kiapo cha uaminifu mbele ya Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.


Wakati wabunge hao wakila kiapo, takribani wabunge 50 wa upinzani walikuwa nje ya ukumbi wa chombo hicho cha kutunga sheria.


Walioapishwa ni Dk Damas Ndumbaro (Songea Mjini), Justin Monko (Singida Kaskazini) na Dk Stephen Kisurwa wa Longido.


Pia, Dk Tulia aliomba wabunge kusimama kwa dakika moja kumkumbuka aliyekuwa mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama ambaye alifariki dunia Novemba mwaka jana.

Na Habel Chidawali, Mwananchi
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post