Sunday, January 28, 2018

Picha : POLISI KATAVI WAUA MAJAMBAZI WAWILI,KUKAMATA WATATU WAKIWA NA SILAHA ZA KIVITA

  Malunde       Sunday, January 28, 2018

Watu wawili wanaodaiwa kuwa ni majambazi wameuawa kwa kupigwa risasi wakati majambazi hao wakijibizana risasi na askari polisi majibishano ya risasi baina yao na askari polisi na wahifadhi ya taifa ya Katavi katika kijiji cha Kapalamsenga wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi.

Pamoja na kuua majambazi hao majambazi wengine watatu kati ya watuhumiwa hao watano wanashikiliwa na polisi baada ya kukamatwa wakiwa na silaha nzito tatu na magazine tano risasi 16 na vipande vinne vya meno ya tembo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 34.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mbele ya  waandishi wa habari na kamanda wa polisi wa mkoa wa Katavi Damas Nyanda alisema tukio hilo  lilitokea jana   majira ya saa sita usiku huko katika kijiji cha Kapalamsenga wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi.

Alisema watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia msako mkali uliofanywa kwa muda wa wiki tatu na jeshi la  polisi na askari wa hifadhi ya taifa ya Katavi ambao walipata taarifa juu ya watu hao kujihusisha na masuala ya ujambazi na ujangili ndani ya hifadhi ya taifa ya Katavi .

Alisema baada ya kupata taarifa hizo ndipo walipo fanya msako huo na kuwasaka watuhumiwa hao na kufanikiwa kuwakamata baada ya mabishano makali ya kurushiana risasi ambapo katika tukio hilo watuhumiwa wawili kati ya watano waliuawa kwa kupigwa risasi .

Alisema watuhumiwa walikamatwa wakiwa na bunduki tatu za kivita aina ya SMG ,risasi 16, magazine tano na vipande vinne vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 6.6 yenye thamani ya Tshs 34,050,000.

Pia watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na nyama ya pofu kilo 20 zenye thamani ya Tshs 3,859,000 wakiwa wamehifadhi ndani ya mfuko wa sandarusi.

Kamanda Nyanda alisema watuhumiwa hao wanaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi utakapokamilika.

Kamanda Nyanda ametoa wito kwa watu waheshimu sheria na waache kufanya uhalifu kwani maisha ya uhalifu ni mafupi na amewataka wananchi wanapoona viashiria vya uharifu watoe taarifa kwenye vyombo husika.

Mkuu wa hifadhi ya taifa ya Katavi Izumbe Msindai alisema ushirikiano wa askari wa hifadhi ya taifa ya Katavi na polisi ndiyo umefanya watuhumiwa hao kukamatwa.

Alisema hifadhi ya Katavi wataendelea kushirikiana na wananchi wanaozunguka hifadhi hiyo katika kukabiliana na suala zima la ujangili wa wanyama ndani ya hifadhi na nje ya hifadhi.

Na Walter Mguluchuma- Malunde1 blog Katavi.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Katavi Damas Nyanda akionyesha vsilaha za kivita walizokamata wakati wakijibizana kwa risasi na majambazi-Picha na Walter Mguluchuma.
Kamanda Damas Nyanda akionyesha magazine tano walizokamatwa nazo watuhumiwa.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Katavi Damas Nyanda akionyesha vipande vya meno ya waliokamatwa navyo watuhumiwa waliokamatwa wakiwa na silaha za kivita 
Kamanda Damas Nyanda akionyesha gobore walilokamata.
Picha na Walter Mguluchuma - Malunde1 blog
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post