MWALIMU MKUU AUAWA KWA KUKATWA MAPANGA


Na Jonathan Musa

Watu wasiojulikana wamemuua kwa kumkata mapanga mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kibumba B,Harun Musiba, iliyopo kata ya Makurugusi wilayani Chato mkoani Geita.

Tukio hilo limetokea usiku wa saa tano wa Januari 13,2018 wakati mwalimu huyo alipotoka kuangalia mpira kati ya Azam na URA ya inchini Uganda uliochezwa jana Zanzibar.

Kamanda wa polisi mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema hawezi kuzungumzia sana kwa kuwa yuko njiani kwenda kwenye tukio na atatoa taarifa zaidi baadae.

Afisa habari wa halmashauri ya Chato Richar Bagolele amesema mwalimu huyo aliwakuta wakata mapanga hao wanamsubiri nyumbani anakoishi ambako ni nyumba ya shule.

Amesema tayari jeshi la polisi wilayani humo limeanza uchunguzi wa tukio hilo.

Matukio ya kukata mapanga katika kanda ya ziwa yamekuwa yakiripotiwa mara kwa mara lakini kwa mkoa wa Geita yalitulia kwa muda sasa.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.