MWAKYEMBE ATOA MAAGIZO MAZITO TFF

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameitaka TFF kuyafanyia kazi malalamiko yote yanayohusu michezo ya ligi daraja la kwanza, kati ya Dodoma FC vs Alliance na Pamba vs Biashara.


Sakata la maamuzi yasiyo ya haki katika michezo ya Dodoma FC dhidi Alliance ya Mwanza na Pamba ya Mwanza dhidi Biashara ya Musoma ndio limefanya Waziri mwenye dhamana ya michezo kutoa agizo hilo kwa shirikisho ili kuhakikisha utata huo unamalizika.


Katika taarifa yake Waziri Mwakyembe ameeleza kusikitishwa na malalamiko ya vitendo vya uonevu na upendeleo katika maamuzi ya mechi hizo huku TFF ikiwa kimya bila kutoa ufafanuzi wa maamuzi hayo.


Mechi hizo zilipigwa Disemba 30 maamuzi yake kugubikwa na utata mkubwa hivyo Waziri amemtaka Rais wa TFF Wallace Karia na viongozi wengine wahusika kuchukua hatua za kuchunguza maamuzi hayo na kuchukua hatua

.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.