MTOBOA MACHO 'SCORPION' ATUPWA JELA MIAKA 7 NA FAINI YA MILIONI 30



Mahakama ya Ilala jijini Dar es salaam leo Jumatatu Januari 22,2018 imemhukumu Mwalimu wa Sanaa ya kujihami, 'Martial arts' Salum Njwete maarufu kama Scorpion, kutumikia kifungo cha miaka saba jela na faini ya Sh milioni 30.



Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Ilala, Flora Haule baada ya Scorpion kupatikana na hatia katika kesi ya kujeruhi ikiwemo kumtoboa macho kinyozi, Said Mrisho.

Hata hivyo mahakama hiyo ilimuachia huru kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha. 

Oktoba 31,2017, Mahakama hiyo ilisema Salum Njwete ana kesi ya kujibu ambayo ni unyanganyi wa kutumia silaha na kujeruhi.

Scorpion alidaiwa kutenda kosa alilohukumiwa nalo Septemba 6,2016 katika eneo la Buguruni Jijini Dar es Salaam. 

Upande wa mashitaka katika kesi hiyo ulikuwa na mashahidi 10 huku Mshitakiwa aliyekuwa akitetewa na Wakili Juma Nassoro alikuwa na mashahidi wawili.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527