MGOMBEA UBUNGE CHADEMA JIMBO LA KINONDONI ARUDISHA FOMU

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Salum Mwalimu, leo Januari 20, 2017 amerudisha fomu za kuwania kinyang’anyiro hicho katika ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi, Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Katika Uchaguzi huo, Mwalimu atachuana na aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), Maulid Mtulia kabla ya kujivua uanachama na kuhamia CCM ambapo ameteuliwa tena na chama chake kupeperusha bendera.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527