MBUNGE SUGU,KATIBU WA CHADEMA WARUDISHWA RUMANDE KESI YA UCHOCHEZI

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini (CHADEMA) Joseph Mbilinyi 'Sugu' na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyassa, Emmanuel Masonga wamerudishwa rumande hadi Januari 22, 2018 siku ya Jumatatu ambapo kesi yake itaanza kusomwa mfululizo. 

Mbunge huyo wa Mbeya mjini na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyassa wanashikiliwa na jeshi la polisi wakituhumiwa kutenda kosa la uchochezi katika mkutano wao wa hadhara ambao ulifanyika Disemba 31, 2017 jijini Mbeya ambapo jeshi la polisi linasema kuwa viongozi hao walizungumza maneno yenye kuleta chuki kati ya Serikali na wananchi. 

Mchana wa January 16, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Jijini Mbeya iliamuru Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyassa Emmanuel Masonga wapelekwe rumande mpaka January 19 ambayo ni leo kwa kesi ya uchochezi. 

Viongozi hao wamerudishwa rumande tena mpaka siku ya Jumatatu ambapo kesi yao itaanza kusomwa tena.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527