LOWASSA AWAVURUGA CHADEMA...LEMA AMFYATUKIA MTANDAONI


Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amemkosoa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwa kauli alizotoa mbele ya Rais John Magufuli.


Lema amemkosoa Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema ikiwa ni saa chache kupita tangu Lowassa alipomtembelea Rais Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.

Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter, Lema ameandika “Mh Lowassa, umeikosea Tanzania kwa kauli baada ya kutoka Ikulu, mema yapi umeyaona katika Serikali hii? Wakati mbunge Lissu (Tundu) bado anauguza majeraha ya risasi.”


“Maiti zinaokotwa, uchumi unaanguka, benki zinafungwa, demokrasia imekufa bungeni /Nje ya Bunge na Sioi mkwe wako bado yuko Magereza,” alihoji Lema ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.

Theme images by rion819. Powered by Blogger.