LOWASSA AMCHANA MTULIA...ATAKA ASIPEWE KICHWA

Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa amefunguka na kuwataka wanachama na viongozi wa CHADEMA kuacha kumtaja taja mgombea Ubunge wa CCM Kinondoni Maulid Mtulia kwani mtu huyo ni wa hovyo hastaili kutajwa tajwa kwani kufanya hivyo ni kumpa kichwa. 

Lowassa amesema hayo jana Januari 27, 2018 akiwa katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa marudio katika jimbo la Kinondoni ambapo leo maelfu ya wananchi wa Kinondoni wameweza kuwasikiliza viongozi mbalimbali wa CHADEMA kwa hoja na sera mbalimbali kuelekea uchaguzi huo ambao unatarajiwa kufanyika Februari 17, 2018. 

"Kwanza nawashauri huyu Mtulia msimseme seme sana wanini huyu, mtu hovyo kabisa huyu mnampa kichwa tu sasa mtu hovyo hapaswi kuchukua muda wenu kumjadili bali nachotaka tushughulike kuwaelimisha wananchi wa Kinondoni kwanini wanastahili kutupa sisi kura, habari ya huyu bwana tuachane naye, hawa CCM hawaeleweki kule Moshi na Korogwe tulishinda lakini wakaja kusema tumeshindwa hivyo nataka kusema saizi tujiandae kulinda kura zetu" alisema Lowassa 

Mbali na hilo Lowassa alimnadi Salum Mwalimu kwa kusema kuwa ni kijana safi ambaye anastahili kwenda Bungeni kuwasemea wananchi wa Kinondoni

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527