KUTANA NA KIJANA HUYU KUTOKA SHINYANGA MWENYE UWEZO MKUBWA WA KUTUNGA VITABU NA HADITHI


Mathayo Methord akielezea kuhusu kipaji cha utunzi wa vitabu na hadithi mbalimbali-Picha na Kadama Malunde1 blog

Kijana Mathayo Methord (21) pichani mkazi wa mtaa wa Magadula kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga mwenye kipaji cha uigizaji na utungaji wa hadithi anatafuta mfadhili na meneja wa kusimamia kazi zake. 

Kijana huyo mwenye kipaji cha hali ya juu cha kutunga hadithi ameiambia Malunde1 blog kuwa ametunga hadhithi zaidi ya 50 lakini ameshindwa kuchapisha vitabu vya hadithi ili kufikia mafanikio yoyote. 

Mathayo Methord ambaye hivi sasa anasoma kidato cha tano katika shule ya Sekondari Old Shinyanga anajiandaa kuchapisha kitabu chake alichokipa jina la “NDOTO ZA MASKINI”,ambacho kinahusu kisa cha kijana maskini aliyekuwa na ndoto ya kufanya makubwa lakini ndoto yake ikazimika baada ya kukutana na misukosuko kadhaa ikiwemo ya mkuu wa mkoa. 

Baadhi ya hadithi alizoziandika na bado hajazichapisha ni pamoja na Dilema,Chozi la Familia,The Saden and Passion,The Real Miracles,Damu za Mashetani,Heat Love,The Magic Wisdom na Ambiguity Love. 

Kijana huyu anatafuta mtu wa kufanya nae kazi pamoja na mfadhili ili aweze kuchapisha hadithi zake ambazo ameziandika. 
Kwa yeyote atakayehitaji kumsaidia kijana huyu ili kutimiza ndoto zake tafadhali wasiliana na Malunde1 blog kwa simu namba 0757 478 553 ,0625 918 527  au wasiliana naye kwa simu namba 0755253804 au mfollow Facebook kwa jina la Scientist Kamu


Theme images by rion819. Powered by Blogger.