WANAUME WANAONUNUA 'MACHANGUDOA' KUSHUGHULIKIWA


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Muliro Jumanne Muliro, amesema wanafikiria kuanza kuwakamata wanaume ambao wananunua wanawake wanaojiuza 'Machangudoa' katika mitaa mbalimbali ya Kinondoni.


Kamanda Muliro ameyasema hayo leo Ijumaa Desemba 29,2017 kwenye kipindi cha East Africa Breakfast cha East Africa Radio ambapo amesisitiza kuwa, kufanya hivyo itasaidia kupunguza wateja na hivyo wadada hawatajiuza tena kwasababu watakosa wateja.

“Nafikiri kama wanaume wangekubali kutokwenda kwa hao madada poa hiyo biashara ingekufa sasa nafikiri badala ya kuwakamata tu hao wadada, wasishangae kwa mkoa wa Kinondoni tukaanza kuwakamata hao wanaume na kuwafikisha mbele ya sheria”, amesema Kamanda Muliro.

Aidha Kamanda Muliro amesema Jeshi la polisi Kinondoni limejipanga kuhakikisha wananchi wakiwemo wafanyabiashara wanafanya shughuli zao kwa amani na usalama kwenye sikukuu ya mwaka mpya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527