Utafiti : WANAUME HUSUMBULIWA MAFUA ZAIDI YA WANAWAKE

Utafiti mpya unaashiria kwamba ni kweli wanaume hutatizwa na mafua zaidi ya wanawake, jambo ambalo limesababisha kuwepo kwa dhana kwamba huwa kuna mafua ya wanaume.

Watafiti nchini Canada wanasema wamepata ushahidi kwamba wanaume hutatizwa zaidi ya mafua ya kawaida na si kwamba huwa wanajifanya kwamba wamezidiwa.

Mtafiti mkuu Dkt Kyle Sue amesema wanaume huenda wana mfumo dhaifu kidogo wa kinga mwilini dhidi ya virusi vinavyosababisha mafua wakilinganishwa na wanawake.

Hilo huenda likawa huchangia kulemewa kwao na dalili za mafua kuliko wanawake.

Dkt Sue anadokeza kwamba wakati umefika pengine kwa wanaume "kutengewa au kutengenezewa maeneo mahsusi, yaliyo na televisheni na viti vizuri, ambapo wanaweza kuuguza mafua yao hadi wapate nafuu bila usumbufu."

Matokeo ya utafiti huo huenda yakafurahiwa sana na wanaume wengi wanaotatizwa na mafua ambao wamehisi kwa muda mrefu kwamba hakujakuwa na watu wa kuwaelewa.

Lakini huenda yasiwafurahishe wanasayansi wengi - na wake pengine - ambao bado wana shaka kuhusu iwapo ni kweli kuna 'mafua ya wanaume' au huwa tu katika fikira za wanaume.
Chanzo- BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post