MVUA KUBWA KUNYESHA SIKUKUU YA KRISMAS NA MWAKA MPYA

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesema wakati wa kuelekea sikukuu za Krismasi na mwisho wa mwaka, mvua kubwa zinatarajiwa kunyesha katika mikoa ya Mbeya, Songwe, rukwa na Kigoma.


Meneja wa kituo Kikuu cha Utabiri wa Hali ya Hewa wa TMA, SAmuel Mbuya, alieleza kuwa mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo ya ukanda wa Pwani ni zile za kumalizika kwa msimu wa vuli.


Mkurugenzi Mbuya alieleza kuwa Mikoa hiyo minne iliyotajwa ndiyo inayotarajiwa kuwa na mvua wakati wa sikukuu na ifikapo mwisho wa mwezi huu, mvua zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali ikiwamo Dar es Salaam zitakuwa zimefikia ukingoni.


“Mvua zinazonyesha maeneo ya ukanda wa Pwani ni zile za vuli na zilianza Oktoba na zinaisha mwisho wa mwezi huu, si mvua zinazoendelea isipokuwa tu katika mikoa ya Mbeya, Songwe Rukwa na Kigoma ambako katika msimu huu wa sikukuu kutakuwa na mvua,” alisema.


Aliongeza kuwa TMA inatarajia mvua zitaendele kunyesha katika mikoa ya. Kigoma, tabora, Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Ruvuma, Lindi, Dodoma na Singida. Alisema mvua katika mikoa hiyo zilianza kunyesha Novemba na zinatarajiwakumalizika mwezi Aprili.


Mbuya aliwataka wananchi kuendelea kufuatilia taarifa zinazotolewa na TMA mara kwa mara, ili kupata mwelekeo wa hali ya hewa pamoja na kuchukua tahadhari mapema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527