MUGABE AONEKANA HADHARANI SINGAPORE

Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu awasili wiki hii nchini Singapore kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake.

Kiongozi huyo aliyekuwa madarakani kwa miaka 37 ameonekana akiwa amezungukwa na walinzi wake huku kwa mbele akionekana mwanamke ambaye inaaminika atakuwa mke wake, Grace Mugabe.

Picha za tukio hilo zinamwonyesha akiwa amevalia shati jeupe na suruali nyeusi wakati mtu anayedhaniwa kuwa mke wake akiwa katika vazi jekundu na beki ya mkononi lenye rangi ya zambarau.

Walinzi wake pia wameonekana kuvalia katika hali ya kawaida ikiwa mashati na suruali. Mara nyingi Mugabe pamoja na walinzi wake wa karibu huonekana wakiwa wamevalia suti isipokuwa wakati alipokuwa akishiriki shughuli za chama au katika sherehe za uhuru.

MWANANCHI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527