Saturday, December 23, 2017

MLINZI AFARIKI KWA KUANGUKIWA TANI 9500 ZA NGANO DAR

  Malunde       Saturday, December 23, 2017Mlinzi wa kampuni ya Amspec, Mwajuma Ibrahimu amefariki dunia baada ya tani 9,500 za ngano kuporomoka ghalani na kumwangukia.


Ghala (silo) hilo lipo Kurasini jijini Dar es Salaam, mali ya kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL).


Kamanda wa Polisi Kikosi Maalumu cha Bandari, Robert Mayala amesema leo Jumamosi Desemba 23,2017 kuwa tukio hilo lilitokea jana Ijumaa Desemba 22,2017 saa 10:00 alfajiri.


Amesema ghala hilo lilipasuka ndipo ngano ilipoporomoka hadi kwenye ofisi aliyokuwamo mlinzi huyo.


Amesema kazi ya kuondoa ngano ili kutoa mwili wa mlinzi huyo inaendelea.

Na Pamela Chilongola, Mwananchi
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post