MKEMIA MKUU : BABA WENGI WALIOPIMA DNA WATOTO SIYO WAO.....BABA FEKI WAMEONGEZEKA


Jumla ya sampuli 72,000 zimepimwa na Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) katika kipindi cha Januari hadi Desemba, mwaka huu na kati ya hizo, 1,177 zilikuwa za vinasaba (DNA) ili kutambua uhalali wa wazazi kwa mtoto na majibu yalibainisha kuwa baba wengi hawakuwa halali.

Akizungumza na Mtanzania Jumapili ofisini kwake juzi, Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele, alisema idadi ya sampuli hizo za DNA zimepatikana katika majalada 338 yaliyowasilishwa katika kipindi cha Januari hadi Desemba, mwaka huu yaliyokuwa na lengo la kufanya utambuzi wa uhalali wa baba kwa mtoto, kesi za jinai, mirathi na utambuzi wa jinsi tawala za mtoto.

“Katika upimaji wa sampuli za kutambua uhalali wa baba kwa mtoto kwa mwaka huu, baba wengi walikutwa si wazazi halali wa watoto waliokuwa wanalalamikiwa,” alisema.

Profesa Manyele alisema idadi ya sampuli hizo kwa mwaka huu zimeongezeka ukilinganisha na mwaka jana ambazo zilikuwa 554 kati ya majalada 332.
Chanzo- Mtanzania Jumapili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527