Makubwa Haya !! MFANYABIASHARA AFANYA SHEREHE KUAGANA NA MARAFIKI ZAKE KABLA YA KUFA

Satoru Anzaki akiwa kwenye karamu hiyo


Mfanyabiashara mmoja nchini Japan ambaye anaugua saratani na anatarajiwa kufariki karibuni amewashangaza watu baada ya kuandaa karamu kubwa ya kuaga.

Satoru Anzaki aliwaalika wageni karibu 1,000 wakiwemo marafiki zake, watu waliosoma naye, washirika wake wa kibiashara na wafanyakazi wake.

Satoru, 80, ambaye ni mkuu wa zamani wa kampuni ya kuunda mashine ya Komatsu alipatikana na saratani ya kibofu cha nyongo Oktoba.

"Nimeridhika kwamba niliweza kusema 'asante' kwa watu niliokutana nao maishani," aliwaambia wanahabari baada ya sherehe hiyo.

"Kwa kuwa nilitaka kufurahia kabisa sehemu ndogo ya maisha niliyobaki nayo, nimeamua nisipokee matibabu baada ya kuzingatia madhara ya tiba," alisema.

Alitangaza mpango wake wa kufanya sherehe hiyo kupitia tangazo gazetini, taarifa ambazo zilisambazwa sana mtandaoni watu wakitaniana kuhusu ingelikuwa wao wangewaalika nani.

Satoru alikodisha chumba katika hoteli moja Tokyo na akaipamba kwa picha za kumbukumbu ya maisha yake.
Chanzo- BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post