WAANDISHI WA HABARI KIGOMA WAPEWA MAFUNZO KUHUSU WAKIMBIZI NA SHERIA MPYA YA HABARI



Afisa uhusiano na mawasiliano,Ofisi ya mratibu mkazi mashirika ya umoja wa mataifa(UN) Didi Nafisa akitoa mada leo Jumatatu Novemba 27,2017 kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) juu mradi wa pamoja wa Kigoma unaofanywa na mashirika 16 ya umoja wa mataifa katika kambi za wakimbizi zilizopo mkoani Kigoma.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wanashiriki katika mafunzo hayo ya siku mbili kuhusu kuripoti habari za wakimbizi na umakini dhidi ya changamoto ya uwepo wa sheria mpya ya habari.Mafunzo hayo yanayofanyika katika ukumbi wa Nzimano Kigoma Mjini yameandaliwa na shirika la umoja wa mataifa(UN)na kuratibiwa na MISATAN Tanzania.Picha zote na Editha Karlo - Kigoma
Kaimu Mkurugenzi MISATAN Tanzania Gasirigwa Sengiyumva akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo hayo
Waandishi wa habari wa Mkoa wa Kigoma kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye mafunzo ya siku mbili kuhusu kuripoti habari za wakimbizi na umakini dhidi ya changamoto ya uwepo wa sheria mpya ya habari mafunzo yaliyoandaliwa na shirika la umoja wa mataifa(UN)na kuratibiwa na MISATAN Tanzania
Wawezeshaji wa mafunzo hayo kutoka kushoto ni Mhariri mtendaji wa The Guardian Jesse Kwayu na James Marenga Wakili kutoka mahakama kuu
Baadhi washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada kwa makini kutoka kwa mwezeshaji Jesse Kwayu (hayupo pichani)

Picha zote na Editha Karlo - Kigoma

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527