SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN LATOA MSAADA WA PIKIPIKI KWA JESHI LA POLISI SHINYANGA


Shirika la kimataifa la Save The Children limetoa msaada wa pikipiki kwa ajili ya dawati la jinsia na watoto la jeshi la polisi wilaya ya Shinyanga kwa ajili ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia. 


Akizungumza leo Ijumaa Novemba 10,2017 wakati wa kukabidhi pikipiki moja kwa jeshi la polisi,Meneja wa shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga Benety Malima alisema pikipiki hiyo itasaidia katika ufuatiliaji wa makosa mbalimbali yakiwemo ya jinai. 

“Shirika letu limekuwa likiendesha mafunzo kuhusu ukusanyaji wa vielelezo kwa ajili ya uchunguzi wa kisayansi kwa ushahidi mahakamani,tumebaini kuwa miongoni mwa changamoto zilizopo ni usafiri,kutokana na hali hiyo tumeona tuangalie namna ya kuwezesha usafiri ili kukabiliana na vitendo vya ukatili katika jamii”,alieleza Malima. 

Akipokea pikipiki hiyo SSP Lutusyo Mwakyusa aliyemwakilisha kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule,alilishukuru shirika hilo kwa kuona umuhimu wa kusaidia jeshi la polisi. 

“Tunalishukuru shirika la Save the Children, huu ni msaada mkubwa sana kwetu kwani utasaidia kuokoa maisha ya watu,na hiki ni kielelezo tosha cha ushirikiano kwa vitendo katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia,naomba wadau wengine waige mfano wa shirika hili ili kujenga jeshi letu la polisi”,alieleza Mwakyusa. 

Aliwataka wadau kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi ili kuhakikisha kuwa matukio ya ukatili yanatokomezwa.
Pikipiki iliyotolewa na shirika la Save The Children kwa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ili itumiwea na dawati la jinsia na watoto kufuatilia matukio ya ukatili wa kijinsia  mkoani Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Meneja wa Shirika la Save The Children Mkoa wa Shinyanga Benety Malima akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi pikipiki kwa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya dawati la jinsia na watoto.
Meneja wa Shirika la Save The Children Mkoa wa Shinyanga Benety Malima akikabidhi funguo ya pikipiki kwa mwakilishi wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SSP Lutusyo Mwakyusa
Meneja wa Shirika la Save The Children Mkoa wa Shinyanga Benety Malima akikabidhi funguo ya pikipiki kwa SSP Lutusyo Mwakyusa
Mwakilishi wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SSP Lutusyo Mwakyusa akijaribu kuendesha pikipiki iliyotolewa na shirika la Save The Children.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527