GARI LA MWENYEKITI WA CCM LAPATA AJALI NA KUJERUHI WATATU




Gari la Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Hussein Mriri limepata ajali katika eneo la Kijiji cha Kikavuchini na kusababisha majeruhi watatu.


Akizungumzia kutokea kwa ajali hiyo leo Jumapili, mwenyekiti wa kijiji cha Kikavu chini, Swaleh Msengesi amesema gari hilo lilikuwa limebeba watu hao waliokuwa katika mkesha wa kuhamasisha wapiga kura usiku wa kuamkia leo Jumapili.


Miongoni mwa waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni Sakra Mtenga ambaye ni mjumbe wa Baraza Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Hai, Veronika Mmboga ambaye ni Diwani Viti Maalum Same na Sophia Sharikiwa, ambaye ni Diwani Viti Maalumu Mwanga.


"Wote wamepelekwa katika hospitali ya Mkoa ya Mawenzi," amesema mwenyekiti huyo.


Na Janeth Joseph, Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post