News Alert : RAIS MAGUFULI AMTEUA DR WILBROAD SLAA KUWA BALOZI




 Rais John Magufuli amemteua Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dkt. Wilbroad  Peter Slaa kuwa balozi.


Taarifa iliyotolewa leo Alhamis Novemba 23,2017  na Ikulu imesema Dkt. Slaa ataapishwa baada ya taratibu zote kukamilika.

Dkt. Slaa ambaye kwa sasa anaishi Canada alitangaza kuachana na siasa kutokana na kutofautiana na chama chake katika kumpokea Edward Lowassa aliyehama kutoka CCM na baadaye kumpitisha kuwa mgombea urais kupitia muungano wa Ukawa.

Dkt. Slaa alisema chama chake hakikutekeleza makubaliano waliyoafikiana ya kuwapokea baadhi ya makada wa CCM akiwemo Lowassa.

Kiongozi huyo alisema anasimamia ukweli na dhamira yake imemfanya ashindwe kumuunga mkono mgombea ambaye amekuwa akimtuhumu kwenye majukwaa.

Alisisitiza kuwa asingehamia chama chochote cha siasa bali angeendelea kutoa mchango wake kwa umma wa Watanzania nje ya vyama vya siasa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post