BODI YA MIKOPO YATOA ORODHA NYINGINE YA WANAFUNZI WALIOPATA MIKOPO


Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) imetoa orodha ya awamu ya tatu ya wanafunzi 7,901 wa mwaka wa kwanza watakaopata mikopo.

Taarifa iliyowekwa kwenye tovuti ya bodi na kuthibitishwa na Meneja Mawasiliano wa HELSB, Omega Ngole imesema hadi sasa wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopata mikopo ni 29,578. Bodi ilisema jumla ya wanafunzi 30,000 watapata mikopo hiyo.

Katika awamu ya kwanza wanafunzi 10,196 wa mwaka wa kwanza walipata mikopo na awamu ya pili wanafunzi 11,481 walipata.

Ngole akizungumza na Mwananchi leo Jumapili Novemba 5,2017 amesema orodha ya wanafunzi waliopata mikopo inapatikana www.heslb.go.tz.

Amesema bado bodi inaendelea kuchambua majina ya wanafunzi wengine walioomba na taarifa zitatolewa baadaye.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.