Angalia Picha : MAHAFALI YA 19 YA KIDATO CHA NNE 2017 SHULE YA SEKONDARI DON BOSCO DIDIA YALIVYOFANYIKA LEO



Wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari Don Bosco Didia mwaka 2017 wakiwa katika mahafali hayo leo-Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog
***
Shule ya Sekondari Don Bosco Didia iliyopo katika kata ya Didia wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga leo Jumamosi Novemba 25,2017 imefanya sherehe ya mahafali ya 19 ya kidato cha nne tangu kuanzishwa kwake ambapo jumla ya wanafunzi 141 wamehitimu masomo yao mwaka huu.

Mgeni rasmi katika mahafali hayo yaliyohudhuriwa na mapadri,masisita,walimu,wanafunzi na wazazi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro. 



Akizungumza katika mahafali hayo,Matiro alisema shule ya sekondari Don Bosco Didia ni miongoni mwa shule zenye sifa nzuri kutokana na wanafunzi wake kuwa na maadili mema lakini pia imeendelea kufanya vizuri katika mitihani mbalimbali. 



“Hii ni shule inayotufanya Shinyanga tutembee kifua mbele kwa sababu inatoa elimu bora na wanafunzi wanalelewa katika maadili yanayotakiwa hivyo kuwa katika mwenendo mzuri”,alisema. 

Matiro aliwaasa wanafunzi waliohitimu elimu ya kidato cha nne kuendelea kuwa waadilifu kwa kufuata mambo mema waliyofundishwa shuleni wanaporudi kwa wazazi wao. 

Aidha alitumia fursa hiyo kuwataka wanafunzi kuzingatia masomo yao badala ya kujiingiza masuala ya mapenzi kwani mapenzi na shule haviendi pamoja. 

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa shule hiyo,Padri Richard Mtui aliwataka wahitimu wa kidato cha nne kubeba mazuri waliyojifunza wakiwa shuleni kwa kipindi cha miaka mitano (Pre form one - Form Four)huku akihimiza kumtanguliza mungu katika maisha yao. 

“Nawakumbusha kumtegemea mwenyezi Mungu,dumisheni shukrani kwani shukrani ni hazina ya moyo,tunategemea pia mtakuwa mabalozi wazuri wa shule hii”,aliongeza. 

Naye Mkuu wa shule hiyo,Padri Mathias Isaka alisema elimu waliyoipata wanafunzi hao itawasaidia kuwa mashujaa,wazalendo,kujisimamia kimaadili,kutetea haki,kukemea ukabili na mambo kadha wa kadha ikiwemo kupambana na dawa za kulevya. 

Padri Isaka alisema hivi sasa shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 1,134 huku akizitaja baadhi ya changamoto zilizopo katika shule hiyo kuwa ni ukosefu wa bweni kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita. 

Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo kwenye mahafali hayo,ametuletea picha 93 za matukio mbalimbali yaliyojiri
Vijana wa skauti kutoka shule ya Sekondari Don Bosco Didia wakimpokea mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (kulia) katika mahafali ya 19 ya kidato cha nne mwaka 2017-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akivalishwa skafu na vijana wa skauti.Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo,Padri Mathias Isaka 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza Mkurugenzi wa shule ya sekondari Don Bosco  Didia,Padri Richard Mtui (katikati) na Padri Thomas Kessy 
Kulia ni Padri Thomas Kessy akizungumza jambo wakati viongozi wa shule ya sekondari Don Bosco wakimpokea mkuu huyo wa wilaya ya Shinyanga
Wahitimu wa kidato cha nne wakijiandaa kuingia ukumbini kwa maandamano
Wahitimu wakiingia ukumbini kwa maandamano
Maandamano kuingia ukumbini...
Mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiingia ukumbini
Walimu,wazazi na wanafunzi wakiwa wamesimama wakati mgeni rasmi akiingia ukumbini
Wahitimu wakiwa wamekaa ukumbini
Wahitimu wa kidato cha nne wakiwa ukumbini
Makamu Mkuu wa shule ya sekondari Don Bosco Didia,Sista Mary Christine akisali wakati wa kufungua sherehe za mahafali hayo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa amekaa na viongozi wa shule hiyo
Mkurugenzi wa shule ya sekondari Don Bosco Didia,Padri Richard Mtui akizungumza katika mahafali hayo
Mwanafunzi Jackline Justine akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wa kidato cha nne
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro,Padri Thomas Kessy na mkuu wa shule Padri Mathias Isaka wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Mkuu wa shule ya sekondari Don Bosco Didia,Padri Mathias Isaka akizungumza katika mahafali hayo 
Padri Mathias Isaka akizungumza ukumbini
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza katika mahafali ya kidato cha nne  shule ya sekondari Don Bosco
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza ukumbini
Wanafunzi wa darasa la Kompyuta (ICT) wakitoa burudani ya wimbo wakati wa mahafali hayo
Wanafunzi wa kidato cha pili wakiimba na kucheza
Wazazi na wageni mbalimbali wakiwa ukumbini
Mahafali yanaendelea
Mahafali yanaendelea
Wazazi wakiwa ukumbini
Wanafunzi wanaobaki wakifurahia jambo
Wanafunzi wa kidato cha kwanza wakiimba wimbo
Mahafali yanaendelea...
Mahafali yanaendelea...
Tupo ukumbini.....
Mahafali yanaendelea...
Mahafali yanaendelea


Wanafunzi wakitoa burudani 
Mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro na viongozi wa shule ya sekondari Don Bosco wakijiandaa kutoa vyeti kwa wahitimu
Mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akimpatia cheti,Rebeca Daudi
Mmoja wa wahitimu akishikana mkono na padri Thomas Kessy
Zoezi la kutoa vyeti kwa wahitimu linaendelea
Wanafunzi wanaobaki wakishuhudia zoezi la ugawaji vyeti kwa wenzao waliohitimu masomo ya kidato cha nne
Zoezi la kugawa vyeti linaendelea..
Wazazi wakiwa ukumbini
Keki kwa ajili ya wahitimu wa kidato cha nne kabla ya kukatwa na kuliwa
Wahitimu wa kidato cha nne,mkuu wa wilaya na viongozi wa shule wakijiandaa kukata keki
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikata keki na walimu na wanafunzi waliohitimu kidato cha nne katika shule ya sekondari Don Bosco Didia
Padri Thomas Kessy akimlisha keki mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro wakati wa mahafali hayo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimlisha keki mmoja wa wanafunzi waliohitimu kidato cha nne
Tunafuatilia kinachoendelea ukumbini...
Wahitimu wa kidato cha nne wakimkabidhi zawadi mkuu wa shule,Padri Mathias Isaka
Wahitimu wa kidato cha nne wakimkabidhi zawadi makamu mkuu wa shule,Sista Mary Christine
Mkurugenzi wa shule Padri Richard Mtui akipokea zawadi kutoka kwa wanafunzi wake
Wazazi na wageni wakifuatilia matukio ukumbini
Mkuu wa shule,Padri Mathias Isaka na Mkurugenzi wa shule Padri Richard Mtui wakipokea zawadi iliyotolewa na wanafunzi hao kwa ajili ya shule
Wahitimu wakiimba wimbo baada ya kutoa zawadi kwa walimu na uongozi wa shule

Wanafunzi wakiimba wimbo


Wanafunzi wakitoa burudani ya kucheza muziki


Wanafunzi wakiimba wimbo

Vijana wakicheza ukumbini
Mkuu wa wilaya akifurahia burudani
Kijana akiimba wimbo ukumbini
Wanafunzi wa kidato cha tano wakicheza wimbo 'Kundi' wa asili wa msanii Bhudagala Mwanamalonja 
Vijana wakionesha kipaji chao cha kuimba
Jinsi ukumbi ulivyofurika....
Kijana akiimba wimbo ukumbini
Wanafunzi wakicheza na kuimba
Burudani ya vijana "Zilipendwa' ikiendelea
Tunafuatilia burudani inayoendelea..

Wazazi wakiwa ukumbini
Mzazi akitoa neno la shukrani wakati wa mahafali hayo
Awali Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisikiliza maelezo kutoka kwa mkandarasi wakati akikagua na kuzindua jengo la Maktaba na madarasa ya kidato cha tano na sita lililojengwa katika shule hiyo kwa msaada wa watu kutoka nje ya Tanzania likigharimu zaidi ya shilingi milioni 250
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiendelea kusikiliza maelezo kuhusu jengo hilo la kisasa
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikata utepe kuzindua rasmi jengo hilo
Padri Thomas Kessy akisali wakati Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizindua jengo hilo
Padri Thomas Kessy akibariki moja ya chumba cha darasa la kidato cha tano katika jengo hilo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia moja ya madarasa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akishuka ghorofani wakati akikagua jengo hilo
Sehemu ya jengo hilo la kisasa kwa ajili ya maktaba na madarasa ya kidato cha tano na sita
Padri Kessy akimwaga maji ya baraka katika chumba cha maktaba
Mkurugenzi wa shule,Padri Richard Mtui akimweleza jambo mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro ndani ya chumba cha maktaba
Padri Thomas Kessy akizungumza jambo nje ya jengo hilo
Picha ya kumbukumbu nje ya jengo hilo
Sherehe za mahafali zilitanguliwa na Misa: Katikati ni padri Thomas Kessy akiongoza misa kuwaombea wanafunzi waliohitimu elimu ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Don Bosco Didia.
Padri Thomas Kessy akiwaombea wahitimu wa kidato cha nne
Wanafunzi wakiwa wamesimama wakati wa misa
Wanafunzi wakifuatilia misa
Misa inaendelea
Mapadri wakiwa wamesimam kwa ajili ya picha ya pamoja na wanafunzi waliohitimu kidato cha nne wakati wa misa hiyo
Wahitimu wa kidato cha nne( wasichana) wakiwa katika picha ya pamoja na mapadri
Wahitimu wa kidato cha nne( wavulana) wakiwa katika picha ya pamoja na mapadri
Wahitimu wa kidato cha nne( wavulana) wakiwa katika picha ya pamoja na mapadri
Walimu wakiwa katika picha ya pamoja na mapadri.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527