WAZIRI WA JPM KUJIUZULU

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameahidi kuwa atajiuzulu nafasi yake endapo tatizo la uvuvi haramu litaendelea kuwa sugu nchini.


Waziri Mpina ameyasema hayo jana walipokuwa akitekeleza lundo la nyavu zinazotumika kwenye uvuvi haramu zenye thamani ya Tsh 30 milioni zilizokamatwa mkoani Kigoma.


Mpina amesema kwamba, endapo atashindwa kutumua dhamana aliyopewa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kukomesha uvuvi haramu atajizulu nafasi yake. Lakini alisema kwamba, hadi kufikia wakati huo ambao atakuwa ameamua kujiuzulu, watu wengine ambao ni wasaidizi wake, nao watakuwa wameumia.


Serikali imepiga marufuku matumizi ya nyavu zenye matundu madogo au uvuvi wa kutumia sumu na baruti ambao husababisha samaki wachanga ambao bado hawajafikia wakati wa kuvuliwa kufa jambo linaloharatisha uwepo wa samaki hao katika miaka ya mbeleni.


Rais Dkt Magufuli wakati akiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi amewahi kuendesha zoezi la uchomaji moto nyavu pamoja na samaki wliovuliwa kinyume na sheria ikiwa ni njia ya kutokomeza uvuvi haramu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527