RAIS MAGUFULI AWASILI ZANZIBAR KWA AJILI YA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU OKTOBA 14,2017

Rais Magufuli leo Oktoba 12, 2017 amekwea pipa na kwenda visiwani Zanzibar akiwa na mkewe Mama kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ambapo Rais Magufuli anategemewa kuwa Mgeni Rasmi siku ya kilele cha Mwenge wa Uhuru Oktoba 14, 2017 Uwanja wa Amaan.


Rais Magufuli visiwani Zanzibar amepokelewa na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.


Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Grayson Msigwa amesema kuwa Rais Magufuli atakuwepo visiwani Zanzibar kwa siku tatu na kudai pamoja na mambo mengine Rais Magufuli atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na siku ya Mwalimu Nyerere.

Theme images by rion819. Powered by Blogger.