MBUNGE WA CHADEMA AANZA KUANIKA USHAHIDI WA RUSHWA YA MADIWANI WAMUUNGE MKONO JPM


Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari ameweka hadharani ushahidi wa rushwa na waliopewa madiwani ambao wamejiuzulu Chadema kwa madai ya kumuunga mkono Rais Magufuli.


Akizungumza na waandishi wa habari leo, Nassari ambaye ameambatana na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema walitoa ushahidi huo na kueleza wataukabidhi Takukuru na katika taasisi nyingine.


Katika ushahidi wa video uliorekodiwa viongozi kadhaa wakiwema Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti pamoja Mkurugenzi Mtendaji wa (H) Meru Christopher Kazeri wamesikika wakiwashawishi madiwani kuhama na baadhi waliahidiwa wangelipwa posho za vikao vyao vilivyobaki hadi 2020 na kukamilishwa miradi yao.


Miongoni mwa makubaliano hayo ni kuwa wapewe fedha na kupata ajira na kukamilishwa miradi yote ya maendeleo waliyoahidi ikiwa ni pamoja na wengine kubadilishiwa makazi pamoja na diwani mmoja kusaidiwa gharama za kufanikisha harusi.


Hata hivyo Mbunge Nassari pamoja na Godbless Lema wameahidi kesho watadfika katika ofisi za TAKUKURU Dar es salaam kwa ajili ya kuukabidhi ushahidi huo wa rushwa kwa Mkurugenzi Valentino Mlowola


Pamoja na hayo wakati Nassari akiutoa ushahidi huo hadharani leo tayari madiwani 10 wa Chama chake wameshapokelewa ndani ya CCM huku wengie wakiwa wamepinga vikali kuhama chama hicho kwa sababu ya rushwa.


Aidha Nassari amesema ameamua kutoa ushahidi huo sasa kwa sababu alikuwa akiendelea kukusanya ushahidi wa kutosha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post