KISHINDO CHA MSIMU WA TIGO FIESTA CHAACHA GUMZO MOSHI


Wasanii Banarba na Gnako wakishiriki uzinduzi wa huduma mpya ya Tigo ya TUMEKUSOMA ambayo ni namba maalum (code number) itakayowawezesha wateja wa Tigo kuingia kwenye menyu na kupata huduma mbalimbali. Uzinduzi huo ulifanyika kwenye tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Majengo Manispaa ya Moshi usiku wa kuamkia Jumatatu. 
Msanii Bright akiwa kwenye jukwaa la Tigo Fiesta liliofanyika uwanja wa Majengo Manispaa ya Moshi 
Chege akiburudisha kwenye jukwaa la Tigo Fiesta liliofanyika uwanja wa Majengo Manispaa ya Moshi 
Msanii Bright akiwa kwenye jukwaa la Tigo Fiesta liliofanyika uwanja wa Majengo Manispaa ya Moshi
Umati wa wakazi wa Moshi wakiwa wanashuhudia burudani iliyokuwa inatolewa na wasanii. 
Gigy Money akiwa katika jukwaa la Tigo Fiesta
Jux akiburudisha wakazi wa Moshi  
****
TIGO Fiesta 2017 imefana vilivyo mkoani Kilimanjaro ambapo wasanii mbalimbali wa Bongo fleva wamefanya vilivyo katika viwanja vya Majengo katika Manispaa ya Moshi kwa kutoa burudani ya kukata na shoka kwa wakazi wa
manispaa hiyo.

Katika kuhakikisha kuwa kila mkazi wa Moshi anafurahia
vilivyo tamasha maalumu la Tigo Fiesta 2017 ambapo mdhamini mkuu wa tukio hilo la aina yake Tigo Tanzania leo wametangaza namba maalumu ya wateja ambayo ni
*147*00# hii inajulikana kama TUMEKUSOMA ambayo wateja wataweza kufanya kuitumia katika huduma
mbalimbali za Tigo.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika tamasha
maalumu la Tigo Fiesta 2017 katika Manispaa ya Moshi, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Tigo Tanzania, William Mpinga alifafanua kuwa, namba hiyo mpya (Code
number) itatumika kwa wateja wa Tigo kote Tanzania katika kupata huduma mbalimbali
za mtandao huo.

Tofauti na matukio  yaliyotangulia, washiriki wote kutoka mtandao wowote kwa tamasha la mwaka huu mbali na kupata huduma ya kulipia kiingilio kwa huduma ya Tigo-Pesa pia wamepata burudani kabambe kutoka kwa wasanii mbalimbali wa muziki kutoka
Tanzania.


Wasanii waliotumbuiza katika Tigo Fiesta katika viwanja vya
Majengo katika Manispaa ya Moshi ni pamoja na Rich Mavoko, Chege, Nandy, Maua, Vanessa, Jux, Ben Pol, Rostam, Weusia, Darassa,Lulu Diva, Rosa Lee, Mimi Mars,
OMG, Gigy Money, Asley na wasanii
wengineo.

Jukwaani Msanii Rosa Ree aliingia kama Malkia na kiti chake
na kuwafanya mashabiki wapagawe na wimbo wake Mchagamchaga na nyingine,

Msanii Aslay kama ilivyokawaida yake mashabiki waliweza
kuimba nae mwanzo mwisho wa nyimbo zake zote, wimbo wake mhudumu ndiyo uliwapagawisha zaidi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya kaskazini, Henry Kinabo amewataka watanzania kutumia huduma mbalimbali zitolewazo na Tigo kwa
kuwa faida inayotokana na huduma inasasaidia huduma mbalimbali za kijamii zikiwemo elimu, afya na nyinginezo ikiwamo mtandao wa intaneti.


“Nawashauri watanzania wote kutumia huduma mbalimbali bora zitolewazo na Tigo kwani sehemu kubwa ya
faida tunayopata tunairudisha kwa jamii kupitia huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo elimu hasa huduma ya intaneti kwashule mbalimbali, mbali madawati tuliyoto
mwaka jana” ,alifafanua Kinabo. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post