ZITTO KABWE: SPIKA WA BUNGE ANATAKA KUFUNIKA NGUVU YA WANANCHI KUHOJI KUHUSU TUNDU LISSU

Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama Cha ACT Wazalendo Mh. Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa Spika wa Bunge Job Ndugai ameibuka sakata lake yeye ili kutaka kufunika nguvu ya wananchi kuhoji juu ya kupigwa risasi Mbunge Tundu Lissu.


Zitto Kabwe amesema hayo leo mara tu baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai leo bungeni kusema anauwezo wa kumzuia Mbunge huyo asizungumze bungeni hadi mwisho wa bunge hilo kwani Zitto hawezi kupambana naye.


"Nimegundua Spika Ndugai ameibua mashtaka yangu ili kufunika ufuatiliaji wa wananchi kuhusu Tundu Lissu kupigwa risasi. Nimeamua sitawapa hilo" aliandika Zitto Kabwe kupitia mtandao wake wa Twitter


Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai jana aliagiza Mbunge Zitto Kabwe pamoja na Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea kufika kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili kuhojiwa kutokana na kauli walizotoa hivi karibuni, jambo ambalo Zitto Kabwe anadai limeibuliwa kwa lengo la kupunguza nguvu ya wananchi kutohoji sakata la Tundu Lissu kupigwa risasi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527