ZITTO KABWE AKAMATWA NA POLISI DAR

Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe amekamatwa na jeshi la polisi leo jioni katika uwanja wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam akitokea Kigoma.


Afisa Habari wa Chama Cha ACT Wazalendo, Abdallah Khamis amethibitisha kukamatwa kwa kiongozi huyo wa chama chake na kusema kuwa kwa sasa wanasheria wa chama hicho wanafuatilia kujua sababu ya kiongozi wa chama chao kukamatwa na jeshi la polisi.


"Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe amekamatwa na Polisi muda huu uwanja wa ndege wa JNIA, Dar es salaam wakati akitoka Kigoma. Kwa sasa wanasheria wa chama wanafuatilia kujua sababu za kukamatwa kwake" alisema Abdallah Khamis.


Asubuhi ya leo kulikuwa na taarifa kuwa Katibu wa Bunge Dkt. Thomas kashililah alitoa amri kwa jeshi la polisi kumkamata Mbunge huyo wa Kigoma Mjini na kutakiwa kumfikisha mjini Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa kutokana na kauli ambazo amewahi kuzitoa juu ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Job Ndugai pamoja na Bunge lenyewe.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post