WATU SABA WAKAMATWA WAKIANDAMANA KUPINGA KIKOMO CHA RAIS UGANDA

Takriban watu saba wametiwa nguvuni katika mji mkuu wa Uganda kampala , kufuatia maandamano ya kupinga mapendekezo ya muswada wa sheria unaoondoa kikomo cha umri wa mtu anayegombea urais.


Katiba ya sasa inasema kikomo cha umri wa urais ni miaka 75.


Mabadiliko ya katiba yatamruhusu rais Yoweri Museveni kugombea tena urais mwaka 2021.


Umri halisi wa rais Museveni haufahamiki, lakini mtandao wa Wikipedia unasema ana umri wa miaka 73.


Wanaharakati vijana wa kundi lijulikanalo kama-The Alternative, ambao waliandaa maandamano hayo, wanasema ofisi yao ilivamiwa jana na wanajeshi pamoja na polisi.


Wanadai laptop, compyuta pamoja na nyaraka nyingine za kampeni yao vilichukuliwa wakati wa uvamizi huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527