WANASHERIA KENYA WALAANI TUNDU LISSU KUPIGWA RISASI

Chama cha Wanasheria nchini Kenya (LSK) kimelaani vikali tukio la kupigwa risasi Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Tundu Lissu.

Rais wa LSK, Isaac Okero amesema tukio hilo limewashtua wanasheria wote wa Kenya.

“Tumepata taarifa kwamba Lissu amepigwa risasi akiwa kwenye gari lake mjini Dodoma, kwa kweli imetushtua sana na inahuzunisha,” amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

“Kwa pamoja tunalaani tukio hilo kwa kuwa hili limewagusa wanasheria wote wa Afrika na hata dunia kwa jumla. Tunasikitika kwa uvunjifu wa sheria uliofanyika,’’ amesema.

Amesema Lissu anafahamika kwa kutetea haki za binadamu, hivyo wanasheria wote wapo pamoja naye katika kipindi hiki kigumu kwake na Mungu atamsaidia atarudi katika hali yake ya kawaida.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post