WANAFUNZI LAKI 9 KUFANYA MTIHANI WA DARASA LA SABA SEPTEMBA 6 NA 7 2017

Wanafunzi 917,072 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi kesho na keshokutwa (Septemba 6 na 7 mwaka 2017).


Kati ya wanafunzi hao, wavulana ni 432,744 sawa na asilimia 47.19, wakati wasichana ni 484,328 sawa na asilimia 52.81.


Watahiniwa 882,249 watafanya mtihani huo kwa lugha ya Kiswahili na 34,823 watatumia lugha ya Kiingereza.


Jumla ya watahiniwa 94 wasioona wamesajiliwa kufanya mtihani huo, wakiwemo wavulana 58 na wasichana 36.


Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde amesema maandalizi yameshakamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa vifaa vinavyohitajika katika halmashauri zote nchini.


Dk Msonde amezitaka halmashauri kuhakikisha utaratibu wa uendeshaji wa mitihani unazingatiwa.


"Tunataka mazingira ya vituo vya mitihani yawe salama, tulivu na kuzuia mianya yoyote inayoweza kusababisha udanganyifu,” amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post