Picha: SHIRIKA LA KIVULINI LAZINDUA MRADI WA 'USAWA WA KIJINSIA,KIUCHUMI KWA WANAWAKE NA VIJANA' SHINYANGA


Ofisa Miradi kutoka Shirika la Kivulini, Eunice Mayengela akiwasilisha kwa wadau mpango mzima wa jinsi mradi huo utakavyotekelezwa katika wilaya za Kishapu na Shinyanga vijijini-Picha na Suleiman Abeid-Malunde1 blog na Mtetezi wa Haki blog
******
Shirika la Kivulini leo Jumanne Septemba 5,2017 limezindua mradi  “Usawa wa Kijinsia kiuchumi wa Kwa Wanawake na Vijana utakotekelezwa kwa kipindi cha miezi sita katika wilaya mbili za Shinyanga vijijini na Kishapu mkoani Shinyanga.

Lengo la mradi huo ni kujenga uwezo, uelewa na mikakati ya kutoa elimu na kuhamasisha jamii kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,mjini Shinyanga,Ofisa mradi kutoka Shirika la Kivulini lenye makao makuu yake jijini Mwanza, Eunice Mayengela Mayengela alisema kutokana na mkoa wa Shinyanga kuwa miongoni mwa mikoa inayokabiliwa na kiwango kikubwa cha ukatili wa kijinsia ikiwemo mauaji ya vikongwe, Shirika la OXFAM kwa kushirikiana na Kivulini wamepanga kutekeleza mradi wa kuhamasisha, usawa wa Kijinsia kujenga uwezo wa kiuchumi kwa wanawake na vijana katika wilaya hizo mbili.

 Alisema mradi huo utatekelezwa katika vijiji vya Nyida, Nsalala, Welezo, Nduguti na Ihalo kata ya Nyida kwa wilaya ya Shinyanga vijijini.

Kwa upande wa wilaya ya Kishapu,alizitaja kata zitakazohusika kuwa ni Talaga, Shagihilu, Uchunga, Lagana na Negezi katika vijiji vya Nhobola, Shagihilu, Ndoleleji, Unyanyembe, Kakola, Mwadulu, Lagana, Bulima, Negezi na Isoso.

Alisema mradi huo utajikita katika kutoa mafunzo juu ya sera na sheria zinazoshughulikia masuala ya ukatili wa kijinsia kwa wawakilishi wa serikali za mitaa, polisi, na watoa huduma wa afya.

Alisema pia kutakuwepo na kampeni ya vyombo vya habari kuhusu sera, sheria na mafunzo iliyopo katika kutetea usawa wa kijinsia pamoja na kujenga uwezo na kuimarisha mfumo wa rufaa wa kushughulikia mashauri ya ukatili wa kijinsia kati ya serikali za mitaa, jeshi la polisi, idara ya afya na mahakama.

"Pia tumelenga kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa njia ya midahalo na sinema, kutoa mafunzo kwa wanamabadiliko ngazi ya jamii (300) ili wafichue na kuchukua hatua za kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia katika maeneo yao", alieleza Mayengela.

Alisema kupitia mradi huo wanatarajia kuongezeka kwa uelewa kwa maskini na makundi maalumu kuhusiana na sheria, sera, na mifumo.

"Kupitia mradi huu ,Kivulini inalenga kuongeza uelewa kwa jamii na serikali za mitaa katika usawa wa kijinsia, sera, sheria na matumizi ya mifumo inayohusiana na kuwasaidia wahanga wa ukatili",alieleza.

"Lakini pia kuwezesha serikali za mitaa kutambua wajibu wao katika utekelezaji wa sera na sheria zinazotetea usawa wa kijinsia katika kumkomboa mwanamke katika ukatili wa kijinsia," aliongeza Mayengela.

Katika hatua nyingine alisema suala la jinsia halimlengi mwanamke au mwanaume pekee, bali linalenga makundi ya watu wote bila kujali jinsi zao ambapo pia ulitolewa ufafanuzi juu ya tofauti ya neno jinsia na jinsi.

Kwa upande wao wadau walishauri pia programu hiyo ikiwashirikishe pia wanaume bila ya kuwabagua na kwamba iwapo utamaduni wa kumtetea zaidi mwanamke utaendelea kuwekewa mkazo ipo hatari katika miaka ijayo kuanzishwa kwa programu nyingine ya itakayolenga kuwatetea wanaume.

Pia walielezea hofu yao kwamba iwapo walengwa wa masuala ya kupiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia watakuwa wanawake na watoto pekee, upo uwezekano wa ndoa nyingi kuvunjika baada ya wanaume kuhisi wanawake hawawajali.
Wadau wakisikiliza kwa umakini mkubwa maelezo ya awali juu ya uzinduzi wa mradi wa Usawa wa Kijinsia kujenga uwezo wa kiuchumi kwa Wanawake na Vijana.
Ofisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Muhoja akifungua rasmi uzinduzi wa mradi huo kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wadau katika kikao cha uzinduzi wa mradi huo.
Ofisa Miradi kutoka Shirika la Kivulini, Eunice Mayengela akiwasilisha kwa wadau mpango mzima wa jinsi mradi huo utakavyotekelezwa katika wilaya za Kishapu na Shinyanga vijijini.

Ofisa Miradi kutoka Shirika la Kivulini, Eunice Mayengela akizungumza ukumbini.


Wadau wakifuatilia kwa umakini maelezo kuhusu utekelezwaji wa mradi huo.
Mdau kutoka kijiji cha Nduguti kata ya Nyida wilayani Shinyanga, Saleh Manota akichangia hoja yake.

Groly Mlaki kutoka Shirika la Kivulini akisherehesha baadhi ya maelezo juu ya utekelezaji wa mradi pamoja na kujibu maswali yaliyoulizwa na wadau. 
Baadhi ya wanahabari wakifuatilia uzinduzi kwa umakini.
Wana habari nao hawakuwa nyuma katika uchangiaji wa mada, Marco Maduhu kutoka gazeti la NIPASHE akitoa mchango wake wa mawazo. 


Washiriki wa uzinduzi wa mradi katika picha ya pamoja.

Picha na Suleiman Abeid-Malunde1 blog na Mtetezi wa Haki blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post