UHURU KENYATTA KUKABILIANA NA MAJAJI WALIOTENGUA MATOKEO YA URAIS WAKE...AHOJI KIVIPI MATOKEO YA URAIS TU??


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa taifa hilo lina 'matatizo' na idara ya mahakama ambayo inahitaji 'marekebisho'.

Alikuwa akizungumza katika hotuba uliopeperushwa moja kwa moja na runinga siku moja tu baada ya mahakama ya juu kubatilisha uchaguzi wake na kuagiza uchaguzi mpya katika kipindi cha siku sitini.

Rais Kenyatta alisema kuwa ataiangazia idara ya mahakama ,mbali na kurejelea ujumbe wake kwamba atauheshimu uamuzi wa mahakama hiyo.

Wameonya kuikabili idara hiyo baada ya uchaguzi.

''Hata iwapo wewe ni mjinga jiulize hivi, matokeo ya uchaguzi wa MCA yalikubaliwa na hakuna mtu aliyeuliza maswali mengi, matokeo ya maseneta na ya wabunge nayo yalitangazwa na tayari wameapishwa na hakuna mtu aliyeuliza maswali. Matokeo ya magavana yalitangazwa na hakuna mtu aliyeuliza maswali ,sasa inakuwaje watu wanne wanaamka na kusema kuwa matokeo ya urais yaliotangazwa yalikuwa na dosari.

Kivipi, kivipi? aliuliza rais Kenyatta katika ikulu ya rais alipokutana na viongozi wa chama cha Jubilee waliochaguliwa.

Rais huyo aliyeonekana kuwa na hasira alionya kukabiliana na majaji hao wa mahakama ya juu atakapochaguliwa.Mkutano wa wanachama wa Jubilee uliofanyika katika Ikulu ya rais

''Tuna matatizo hapa. Mwanzo ni nani aliyewachagua? tuna tatizo na lazima turekebishe'', alisema.

Amesisitiza kuwa ijapokuwa anaheshimu uamuzi wa mahakama hiyo ya juu na kwamba alikuwa tayari kushiriki katika uchaguzi mwingine alisema kuwa uamuzi wa mahakama hiyo ulikuwa na makosa.

''Mahakama ya juu iliketi chini ikaamua kwamba hiyo ndiyo yenye nguvu zaidi ya Wakenya milioni 15 walioamka alfajiri na kupanga foleni na kumpigia mgombea wa urais waliomtaka''.Rais Uhuru Kenyatta akiwahutubia viongozi wa chama tawala ha Jubilee siku moja baada ya uchaguzi wake kubatilishwa na mahakama.

''Mahakama ya juu haiwezi kufutilia mbali maono ya Wakenya.Na tutaliangazia swala hili.Niangalieni machoni na museme iwapo upendo wangu wa Wakenya kuishi kwa amani ndiyo unaonekana kuwa uoga, hatuogopi''.

Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post