MWANDISHI WA HABARI NGULI NA ALIYEWAHI KUWA DC AMEFARIKI DUNIA

Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni (2012), wilaya ya Morogoro na nguli wa habari nchini, Rweyemamu Muhingo(67) amefariki leo katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam. 

Muhingo ameacha simanzi katika tasnia ya habari, familia na taifa kwa ujumla.

Muhingo ambaye awali alibahatika kuteuliwa na Rais wa Awamu ya nne, Jakaya Kikwete kuongoza wakazi wa Halmashauri ya Handeni kabla ya kuhamishiwa Makete na baadaye Morogoro mjini. 

Kabla ya uteuzi huo, aliwahi kuwa mwandishi wa habari gazeti la Mwananchi linalochapisha magazeti ya Mwanaspoti na The Citizen. Pia aliwahi kuandikia gazeti la Mtanzania 

Mtoto wa marehemu, Mwesigwa Muhingo ameliambia gazeti hili leo kwamba, amefariki kwa maradhi ya Myelofibrosis, yanayotokana na mifupa kushindwa kutengeneza damu. 

“Alhamisi tulikuwa na mpango wa kumsafirisha nje ya nchi ingawa tulikuwa hatujapata hospitali hali yake ilibadilika ghafla leo saa 3:00 Mungu akamchukua’’amesema Muhingo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post