UHURU KENYATA ASEMA HAKUBALIANI NA UAMUZI WA MAHAKAMA LAKINI ANAUKUBALI...KAWAHIMIZA WAKENYA KUDUMISHA AMANI

Mahakama ya juu nchini Kenya imefuta ushindi wa Rais Uhuru Kenyata kwa uchaguzi uliofanyika Agosti 8, 2017, na kutaka uchaguzi huo urudiwe.

Hukumu hiyo imetolewa leo na jopo la majaji 6 ilirushwa moja kwa moja kwenye vyombo vya habari nchini Kenya, imesema uchaguzi huo utarudiwa baada ya siku 60. 

Akisoma uamuzi huo Jaji Mkuu David Maraga amesema tume ya uchaguzi ilikiuka Katiba na Sheria katika baadhi ya mambo na hivyo kuathiri matokeo ya uchaguzi. 

Akihutubia taifa la Kenya baada ya uamuzi huo wa mahakama,Rais Uhuru Kenyatta  amewahimiza Wakenya kudumisha amani.

"Jirani yako atasalia kuwa jirani, bila kujali mrengo wao wa kisiasa, dini, rangi".

Amesema hakubaliani na uamuzi uliotolewa na mahakama, lakini anaukubali.

"Watu hao sita (majaji) wameamua kwamba wataenda kinyume na mapenzi ya watu. Nyinyi Wakenya mlichagua wabunge wengi wa Jubilee, maseneta wengi wa Jubilee na wawakilishi wa wanawake wa Jubilee, wawakilishi wengi wa wadi wa Jubilee," amesema.

"Tuko tayari kurudi tena kwa wananchi, tukiwa na ajenda ile ile tuliyowasilisha, ajenda ya kuunganisha nchi. Kuunda chama cha taifa. Kuendeleza nchi hii.

"Hatuko kwenye vita na ndugu zetu wa upinzani.

"Tuko tayari kurudi kwa debe, kuongea na Wakenya, kuwaambia yale tunataka na yale tunataka kutenda."

"Watu wachache, watu sita, hawawezi kubadilisha nia ya Wakenya milioni 40. Wakenya ndio wataamua, na hivyo ndivyo demokrasia ilivyo."
Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post