NYUMBA YA ZITTO KABWE YATEKETEA KWA MOTO

Nyumba ya Mbunge Kigoma Mjini Zitto Kabwe iliyopo Kibingo, Kata ya Mwandiga mjini Kigoma imeungua moto jioni ya leo ambapo mpaka sasa chanzo cha moto huo hakijafahamika.

Hayo yamethibitishwa na Afisa habari wa chama cha ACT, Abdalla Khamis na kusema ni kweli tukio hilo limetokea lakini siyo katika nyumba ambayo anaishi Mbunge Zitto Kabwe.

"Ni kweli nyumba ya Zitto imeungua moto jioni ya leo lakini siyo nyumba ambayo anaishi yeye binafsi, bali ni nyumba ambayo imejengwa katika kiwanja kimoja na nyumba anayoishi kwa sasa", amesema Abdalla.

Kauli ya Zitto Kabwe:

Tumepata ajali kidogo. Nyumba yangu ninayoishi katika eneo la Kibingo, mji mdogo wa Mwandiga, Kigoma imeteketea kwa moto jioni hii. Alhamdulillah, kuwa hakuna binaadam aliyeumia.


Nawashukuru Jeshi la Zimamoto, majirani zangu pamoja na wananchi wenzangu kwa ushirikiano walioutoa mpaka kuuzima moto husika. Kwa sasa Jeshi la Polisi wanafanyia kazi kujua chanzo cha ajali.


Naomba wananchi wewe watulivu wakati Polisi wanaendelea na uchunguzi husika.

Nairobi - Kenya
Septemba 16, 2017


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post