MBUNGE WA CCM JOSEPH MSUKUMA AKAMATWA NA POLISI

Mbunge wa Geita Joseph Kasheku Msukuma amekamatwa na Polisi mkoani humo, kutokana na tuhuma za kuhusika kwa tukio la kufungwa kwa njia kwenye barabara ya kuelekea kwenye mgodi wa GGM wiki iliyopita.


Akithibitisha kukamatwa kwa mbunge huyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo alipokuwa akionga na mwandishi wa habari wa East Africa Television, amesema Musukuma amekamatwa leo baada ya kupata taarifa kuwa anahusika na tukio hilo.


"Ni kweli Mbunge Musukuma tumemkamata leo kufuatia tukio la juzi" amesema Kamanda Mwabulambo.


Pia Kamanda Mwabulambo amesema mpaka sasa wanawashikilia watu 8 ambao 6 miongoni mwao ni madiwani wa kata mbali mbali mkoani humo, na watafikishwa kwenye vyombo vya sheria kama ambavyo inatakiwa.


Siku ya Alhamisi ya Septemba 14, 2017, wananchi mkoani Geita walifunga barabara inayoingia katika mgodi wa GGM kushinikiza malipo ya kodi ya dola 12.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527