JESHI LA POLISI KANDA MAAALUM YA DAR ES SAALAM LAAGIZWA KUKOMESHA UKATILI WA KIJINSIA

Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan amemtaka Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamanda Lazaro Mambosasa kuhakikisha kanda yake inatokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.

Mama Samia ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam katika Tamasha la 14 la Jinsia lililofanyika katika viwanja vya TGNP Mabibo.

“Bado takwimu za Jeshi la Polisi zinaonyesha ukatili wa kijinsia unaendelea. Kamanda Mambosasa tunakuachia wewe suala hili, likitokea tunakubana wewe na wewe utawabana wenzako,” alisema.

Mama Samia alisema serikali inaendelea kutekeleza Mpango mkakati wake wa miaka mitano wa kutokomeza ukatili wa jinsia ili kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto unapungua kwa asilimia 50.

“Bila wanawake kuzitumia sera na sheria za wanawake na jinsia zilizotungwa na serikali hatutafanya lolote. Isipokuwa tutazifungia na kuziweka katika makabati na hatutafika kokote,” alisema.

Hata hivyo, Mama Samia alisema serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuwakomboa wanawake ikiwemo kufufua Benki ya Maendeleo ya Wanawake nchini (TWB).

“Serikali imechukua hatua mbalimbali kumkomboa mwanamke kiuchumi ili aweze kusaidia jitihada za serikali za kuleta maendeleo. Tuna Mpango wa kufufua benki ya wanawake, ni wajibu wenu kuhakikisha haifi. Watu wenye uwezo waisaidie serikali kuitafutia mitaji,” alisema.

Aidha, Mama Samia aliwataka wanaume kutowanyanyasa wanawake kwa kuachana na mila na desturi potofu zinazokandamiza haki za wanawake na jinsia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post