HATIMAYE HAMISA MOBETTO AWEKA MAMBO HADHARANI

Mwanamitindo Hamisa Mobetto ameamua kuweka mambo hadharani kwa kumtaja baba wa mtoto wake wa pili AbdulLatif kuwa ni Diamond Platnumz.


Kwa mujibu wa akaunti ya mtandao wa Instagram ya mtoto huyo inaonyesha jina kamili la mtoto kuwa ni “Dully Dangote (AbdulLatif Naseeb Abdul Juma )Lion 🦁 (Leo) -8|8|2017 TanzanianBaby 👑 @hamisamobetto & Diamond Platnumz Son.”


Miezi kadhaa nyuma Diamond Platnumz alikuwa akikana kuhusika kutoka kimapenzi na mwanamitindo huyo na pia kukana mimba aliyokuwa nayo mrembo huyo.


Hamisa ambaye alianza kutaja majina ya baba wa mtoto huyo miezi kadhaa nyuma kwa herufi za mwanzo, hatimaye ameweka jina lote la baba huyo katika akaunti ya mtandao wa kijamii wa Instagram.


Abdullatif ni mtoto wa pili wa mrembo huyo ambapo mtoto wa kwanza Fantasy alizaa na Mkurugenzi wa EFM, Majay.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527