Picha: DEREVA WA MBUNGE WA CHADEMA AKATWA SHOKA KICHWANI NA WATU WASIOJULIKANA


Dereva wa Mbunge John Heche (CHADEMA) amevamiwa usiku wa kuamkia leo Ijumaa Septemba15,2017 na watu wasiojulikana na kukatwa na shoka kichwani Mjini Tarime na anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime. 

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa mbili usiku ambapo dereva huyo anadaiwa kukatwa na shoka kichwani. 

Mbunge John Heche amethibitisha kutokea kwa tukio hilo kutokana na taarifa alizopata kupitia Katibu wake, Mrimi Zabron ambaye amekiri Dereva huyo anayefahamika kwa  jina la Suez Daniel Maradufu ni kweli amepata shambulio hilo na sasa yupo hospitali akipatiwa matibabu. 

Kwa upande wa Kamanda wa Polisi Tarime Rorya, SACP Henry Mwaibambe alipotafutwa kwa njia ya simu na Mwandishi wetu amesema yupo kwenye kikao na akimaliza atatoa ripoti kamili. 
Suez Daniel Maradufu ambaye ni Dereva wa Mbunge jimbo la Tarime Vijijini CHADEMA John Heche akiwa amelazwa katika Wodi namba tatu kwa ajili ya Matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime Mkoani Mara. 

Mrimi Zabron ambaye ni katibu wa Mbunge wa jimbo la Tarime Vijijini John Heche akimjulia hali Dereva wa Mbunge huyo katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527