CHADEMA: HATUNA IMANI NA UCHUNGUZI UTAKAOFANYWA NA POLISI AU SERIKALI KUHUSU TUNDU LISSU


Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara na Wakili wa kujitegemea Tanzania. Prof Abadallah Safari amesema wao kama CHADEMA hawana imani na uchunguzi utakaofanywa na jeshi la polisi au serikali kuhusu shambulio la kujaribu kumuua Mbunge Tundu Lissu.


Akizungumza na wanahabari wakati wakitoa taarifa ya kamati kuu kupitia kikao walichokaa mwishoni mwa wiki iliyopita, Prof. Safari amesema kuwa wao hawana nia mbaya ya kutaka uchunguzi kufanywa na wachunguzi wa mambo ya nje lakini hii ni kutokana jinsi tukio lilivyotokea.


"Hatuna nia mbaya lakini sisi kama CHADEMA hatuna imani na serikali pamoja na jeshi lake la polisi katika uchunguzi wa jaribio la mauaji ya Mbunge wetu. " alisema Prof Safari.


Pamoja na hayo Prof. Safari amedai anamshangaa sana Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini , IGP Simon Sirro, kwa kauli yake ya kwamba Tundu Lissu hakufika kuripoti tukio la kufuatiliwa na watu asiowajua na kusema kuwa huko ni kutojua sheria ya mmwenendo wa makosa ya jinai.


Amesema kuwa Sheria hiyo inaeleeza namna jeshi lapolisi linavyotakiwa kufanya kazi zake na kwamba jeshi la polisi kazi yake ni kufuatilia na kufanya upelelezi juu ya taarifa kwani wao ni walinzi wa amani na kuongeza kwamba Lissu tayari alieleza kila kitu lakini polisi hawakujali.


"Hatuamini kama walikuwa hawajui kama kuna taarifa Lissu alizitoa kuhusu yeye kufuatiliwa au waliamua tuu kutotilia maanani" alisisitiza Prof. Safari.


Mbali na hayo Katibu Mkuu wa Chama hicho Dkt. Vicent Mashinji ameeleza kwamba kwa sasa wanachohakikisha ni kwamba hospitali aliyopo Lissu inazidi kuimarishwa ulinzi lakini pia hatoweza kuzungumzia hali yake kwa undani kutokana pia na kuwepo watu wasiokuwa na nia njema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527