YANGA YATOKA SARE NA LIPULI FC

Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara leo Jumapili Agosti 27,2017 imeendelea kwa mchezo mmoja kati ya Yanga na Lipuli Fc.


Mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam umemalizika kwa sare ya kufungana goli moja kwa moja.


Lipuli ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata gori kupitia kwa mchezaji Seif Abdalah Karihe kunako dakika ya 44 ya kipimdi cha kwanza.

Dakika 45 ya kipindi cha kwanza Donald Ngoma aliisawazishia goli na kufanya kuwa moja moja.

Mpaka wanaenda mapumziko matokeo ni moja moja.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kubwa ambapo yanga walionekana kuliandama lango la Lipuli mara kadhaa,hali hiyo haikuzaa matunda yeyote kwani mpaka kipenga cha mwisho cha mwamuzi kinapulizwa matokeo yakibaki yale yale ya 1-1.

Full time Yanga 1-1Lipuli

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post