TUNDU LISSU ARUDISHWA POLISI BAADA YA POLISI KUFANYA UPEKUZI NYUMBANI KWAKE

Jeshi la Polisi limemaliza zoezi la kufanya upekuzi katika nyumba ya Mwanasheria Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyopo Tegeta Dar es Salaam na baada ya hapo Lissu amerejeshwa Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.


Jeshi la polisi lilikwenda nyumbani kwa Tundu Lissu kufanya ukaguzi kufuatia makosa mawili ambayo Mbunge huyo wa Singida Mashariki na Rais wa TLS anatuhumiwa nayo ambayo ni pamoja na Kusema makosa ya Rais John Pombe Magufuli hadharani na chochezi kuhusu kushikiliwa ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 huko nchini Canada.


Kwa mujibu wa Afisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene amedai kuwa Tundu Lissu amerudishwa Kituo Kikuu cha Polisi kwa ajili ya taratibu zingine za kisheria ambazo zitaendelea ikiwa pamoja na dhamani ambayo kisheria ipo wazi.


Tundu Lissu alikamatwa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2017 na jeshi la polisi alipotoka mahakamani kwenye kesi ya uchochezi , alipelekwa Police Central kwa ajili ya kufanyiwa mahijiano na baadaye kulala rumande kutokana na jana kushindwa kupewa dhamana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post