SHERIA MPYA YA VYAMA VYA SIASA YAJA...SASA WADAU KUTOA MAONI


OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa imeanzisha tena mchakato wa kupokea maoni ya ziada kutoka kwa wadau vikiwemo vyama vya siasa kwa lengo la kuboresha mfumo usajili na uratibu wa shughuli za vyama vya siasa.

Akizungumza na gazeti la Habarileo jana, Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza ofisi yake imeuhisha mchakato huo tena baada ya ule ulioanza mwaka 2013 kusitishwa kupisha mchakato wa utungwaji wa Katiba na Uchaguzi Mkuu uliopita.

“Wazo la kutungwa sheria mpya ya vyama vya siasa ilitokana na maoni ya wadau walioeleza kuwa sheria ya sasa ina mapungufu, na mwaka 2013, tulipokea maoni kutoka kwa vyama vya siasa na asasi za kirai, sasa tumewataka wadau kutuma maoni ya ziada kama wanayo,” alisema Nyahoza.

Alipoulizwa ni maeneo gani ambayo wamelengwa kuboresha, Nyahoza alisema kwa sasa hawezi kubainisha maeneo hayo na kuwa wametoa fursa kwa wadau kubainisha maeneo yenye upungufu.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imewaandikia wadau vikiwamo vyama vya siasa na asasi za kiraia ikiwataaka kupeleka maoni ya ziada baada ya ofisi hiyo kupendekeza kutungwa kwa sheria mpya ya vyama vya siasa nchini.
Chanzo-Habarileo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527