RAIS WA NCHI : KILA MTU LAZIMA APIMWE UKIMWI

Rais wa Zambia Edga Lungu amesema kuwa kwa sasa ni lazima kila mtu apimwe hali yake ya ugonjwa wa ukimwi nchini humo.

Zambia ni kati ya nchi zenye viwango vya juu zaidi vya ukimwi kusini mwa bara la Afrika kwa asilimia 11.6, huku watu walio na umri wa kati ya miaka 15 na 49, wakiwa na wanaishi na virusi vya ukimwi.

Bwana Lungu alisema kuwa kupimwa na kupewa ushauri na matibabu sio kitu cha kujitolea, katika jitihada za kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi nchimi humo.

Alitoa tangazo hilo wakati wa uzinduzi na baraza la ukimwi kwenye mji mkuu Lusaka.
Bwana Lungu alisema kuwa suala hilo limezungumziwa na baraza la mawaziri.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post